Mzee 72, afariki baada ya kunywa pombe

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 72 aliaga dunia baada ya kudaiwa kubugia pombe kupindukia katika eneo la matunda kaunti ndogo ya Likuyani.

Akithibitisha kisa hiki kinara wa polisi katika kaunti hiyo ndogo, Meshack Kiptum alisema mwili wa mzee huyo ambaye hajatambulikana ulipatika jana alfajiri katika soko la matunda.

Mwili wake uliondolewa na polisi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya Kitale huku polisi wakianzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.

Kiptum ametoa wito kwa yeyote ambaye huenda amempoteza jamaa wake wa kiume mwenye umri wa umri kama huo kujitokeza na kusaidia kuutambua mwili huo.

Na Maurice Aluda